Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Septemba 28, 2022 Local time: 10:34

Jenerali Chiwenga huenda akateuliwa makamu wa rais Zimbabwe


Jenerali Constantino Chiwenga. Shirika la habari la Reuters liliripoti kwamba rais Emerson Mnangagwa atajaza nafasi za manaibu wawili wa rais na Chiwenga huenda akawa mmoja wao.

Mkuu wa jeshi la Zimbabwe anaonekana kama atakayeteuliwa kuwa makamu wa rais baada ya serikali kutangaza Jumatatu kuwa atastaafu wakati akingojea uteuzi mpya.

Jenerali Constantino Chiwenga aliongoza mapinduzi yaliofikisha ukingoni utawala wa miongo kadhaa wa Robert Mugabe.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, rais Emmerson Mnangagwa amesema atajaza nafasi za manaibu wawili wa rais katika kipindi cha siku chache zijazo.

Mnangagwa tayari ameteua maafisa wakuu wa jeshi kadhaa kwenye baraza lake la mawaziri tangu alipoapishwa kuwa rais Novemba 24.

Alimteua generali Edzai Chimonyo aliyekuwa balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania kuchukua nafasi ya kamanda wa jeshi la nchi kavu kutoka kwa kamanda Phillip Sibanda anayetarajiwa kuchukua nafasi ya Chiwenga.

Wakati huo huo, serikali imetangaza kustaafu kwa mkuu wa polisi Augustine Chiruri ambaye anasemekana kuwa mshirika wa karibu wa rais wa zamani, Robert Mugabe.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG