Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 20:48

China yawekea vikwazo kampuni mbili za Marekani za masuala ya ulinzi


Rais wa China Xi Jinping

Wizara ya biashara ya China, Alhamisi imetangaza kuziwekea vikwazo kampuni mbili za Marekani za masuala ya ulinzi kwa kuiuzia Taiwan, silaha, ambapo imezipiga marufuku kuingiza bidhaa China ama kufanya uwekezaji wowote na taifa hilo.

Hatua hiyo imechukuliwa ikiwa ni zaidi kidogo ya wiki moja baada ya China kuahidi kujibu mapigo kwa Marekani, baada ya kutungua puto ambalo linaaminika kufanya upelelezi ambalo liliruka katika sehemu kubwa ya Marekani.

Katika taarifa, wizara ya biashara ya China, imesema kampuni za Lockheed Martin Corp, na Raytheon Technologies Corp, na kitengo chake cha makombora na ulinzi kwa pamoja vimepigwa marufuku kujihusisha na uingizaji ama usafirishaji unaohusiana na China ama kufanya uwekezaji wowote mpya nchini humo.

Kampuni zote hizo zinakatazwa na sheria za Marekani kuuza silaha zinazohusiana na teknolojia za China.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG