Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 05, 2024 Local time: 16:39

China yatoa tahadhari kwa wanainchi wake kufuatia ongezeko la ugonjwa wa kupumua


Watoto na wazazi wao wakisubiri kwenye eneo la wagonjwa wa nje kwenye hospitali ya watoto mjini Beijing, Novemba 23, 2023.
Watoto na wazazi wao wakisubiri kwenye eneo la wagonjwa wa nje kwenye hospitali ya watoto mjini Beijing, Novemba 23, 2023.

China leo Ijumaa imetoa wito wa tahadhari kwa wananchi wake huku ugonjwa wa kupumua ukiongezeka na kuziathiri shule na hospitali.

Shirika la afya duniani (WHO) ambalo limeitaka serikali kutoa takwim kuhusu ugonjwa huo limesema hakuna vimelea visivyo vya kawaida vilivyogunduliwa.

China inakabiliwa na ongezeko la ugonjwa wa kupumua huku ikiingia katika msimu wake kamili wa baridi tangu ilipoondoa masharti makali ya Covid 19 mwezi Disemba mwaka jana, huku visa miongoni mwa watoto vikionekana kuongezeka hasa katika maeneo ya kaskazini kama vile Beijing na jimbo la Liaoning.

Baraza la serikali limesema kuwa flu itafikia kilele msimu huu wa baridi na masika na maambukizi ya homa ya mapafu yataendelea kuongezeka katika baadhi ya maeneo siku zijazo.

Lilionya pia juu ya hatari ya kuibuka tena kwa maambukizi ya Covid.

Forum

XS
SM
MD
LG