Msemaji wa wizara ya ulinzi Kanali Tan Kefei, anasema ongezeko la hivi karibuni la mabadilishano kati ya wanajeshi wa Marekani na Taiwan ni hatua mbaya na hatari sana.
Tan anasema Jeshi la ukombozi la watu wa China linaendelea kuimarisha mafunzo na maandalizi ya kijeshi ili kukabiliana na vikosi vinavyounga mkono uhuru na uingiliaji kutoka nje, akimaanisha mshirika wa karibu wa Taiwan, Marekani.
China inadai kisiwa hicho chenye watu milioni 23 kuwa ni eneo lake na kinapaswa kuwa chini ya udhibiti wake kwa nguvu kama itatakiwa kufanyika hivyo.