Jenerali Li Shangfu, ambaye hakuonekana hadharani kwa miezi miwili, amefutwa kazi kama waziri wa ulinzi na diwani wa serikali, kulingana na vyombo vya habari vya serikali.
China ilitangaza pia kwamba Qin Gang, ambaye alifutwa kazi kama waziri wa mambo ya nje mwezi Julai, aliondolewa pia kwenye uadhifa wake wa diwani wa serikali.
Atakayechukua nafasi ya Li hakuteuliwa, na kuiacha nchi bila waziri wa ulinzi inapojiandaa kuwa mwenyeji wa mkutano wa mawaziri wa ulinzi kutoka mataifa ya kigeni mjini Beijing Oktoba 29 hadi Oktoba 31.
Forum