Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 13, 2024 Local time: 11:29

China yalalamikia vikali ziara ya Pelosi, Taiwan


Spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi akitembelea majengo ya bunge mjini Taipei, Taiwan
Spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi akitembelea majengo ya bunge mjini Taipei, Taiwan

China Jumanne imelalamikia  balozi wa Marekani mjini Beijing Nicholas Burns, kutokana na ziara ya spika wa bunge la Marekani Nancy Pelosi kwenye kisiwa cha Taiwan kulingana na chombo cha habari cha serikali.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, naibu waziri wa mambo ya kigeni wa China Xie Feng amelalamika vikali ziara ya Pelosi kwenye kisiwa hicho kinachojitawala, na ambacho China inadai kumiliki, wakati akifanya mazungumzo ya moja kwa moja na Burns.

Shirika la Xinhua limemnukuu Xie akisema kwamba, "Ziara hiyo ni ya kichokozi na kwamba mathara yake ni makubwa", akiongeza kusema kwamba China haitatazama tu bila kuchukua hatua. Ziara ya Pelosi ndiyo ya kwanza ya afisa wa ngazi ya juu zaidi wa Marekani ya Taiwan ndani ya miaka 25, na tayari imeongeza taharuki kati ya mataifa yote mawili yanayoongoza kiuchumi ulimwenguni, na kutajwa na Beijing kuwa ya kichokozi.

Xie ameonya kwamba Marekani italipia makosa yake, wakati akiomba Washington kuchukua hatua mara moja kuepusha mathara yalioletwa na ziara hiyo. Pelosi aliwasili Taiwan Jumanne jioni licha ya onyo kutoka Beijing.

XS
SM
MD
LG