Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 15, 2024 Local time: 13:43

China yaitaka Ufilipino kuondoa meli ya kivita iliyotelekezwa katika eneo lenye mzozo


Meli ya walinzi wa pwani ya Ufilipino ikifanya doria karibu na meli ya jeshi la majini iliyotelekezwa BRP Sierra Madre, April 23, 2023. Wanajeshi wa majini wa Ufilipino wamewekwa ili kuthibitisha madai ya Manila ya Kisiwa cha Second Thomas Shoal.
Meli ya walinzi wa pwani ya Ufilipino ikifanya doria karibu na meli ya jeshi la majini iliyotelekezwa BRP Sierra Madre, April 23, 2023. Wanajeshi wa majini wa Ufilipino wamewekwa ili kuthibitisha madai ya Manila ya Kisiwa cha Second Thomas Shoal.

China inaitaka Ufilipino kuondoa meli ya kivita iliyotelekezwa katika sehemu inayokaliwa kutoka kwenye eneo lenye mzozo katika Bahari ya South China.

Madai yaliyotolewa Jumanne na Beijing yamekuja siku tatu baada ya meli ya walinzi wa pwani ya China kupiga mzinga wenye nguvu wa maji kuelekea meli za kijeshi za Ufilipino zilizokuwa zinaelekea katika eneo la Second Thomas Shoal kwa lengo la kupeleka mahitaji.

Manila ilisema vitendo vya walinzi wa pwani ya China vilizuia moja ya boti mbili zilizokuwa zinapeleka mahitaji kushindwa kupakua mahitaji ya dharura kwa ajili ya majeshi ya Ufilipino yaliyoko katika meli ya kivita ndefu yanayo linda eneo hilo la Shoal.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China ilitoa tamko ikiitaka Ufilipino kuondoa mara moja meli iliyoegeshwa kutoka eneo la Second Thomas Shoal na kuiweka katika eneo la zamani ambalo halikaliwi kimabavu.

Lakini Jonathan Malaya, msemaji wa Baraza la Usalama la Taifa la Ufilipino, aliwaambia waandishi Jumatatu kuwa Ufilipino “ kamwe haitaondoka katika kituo chake huko Ayungin Shoal,” akitumia jina la kisiwa hicho ambacho ni Second Thomas Shoal.

Tukio hilo ni mvutano wa hivi karibuni kabisa katika mgogoro wa kieneo uliokuwa unafukuta kwa muda mrefu ukizihusisha China, Ufilipino, Vietnam, Malaysia, Taiwan na Brunei katika Bahari ya South China.

China inadai umiliki wa takriban eneo la kimkakati la njia ya maji licha ya uamuzi wa kimataifa uliobatilisha madai ya umiliki wa eneo kubwa yaliyodaiwa na Beijing, kama yale ya mwaka 2016 yaliyofanywa na Mahakama ya Kudumu ya Usuluhishi, Taasisi ya kimataifa iliyoko The Hague.

Mivutano kati ya China na Ufilipino juu ya Bahari ya South China imeongezeka tangu Rais Ferdinand Marcos, Jr. alipoingia madarakani mwaka jana na kuirejesha Manila kwa mshirika wake wa muda mrefu Marekani, akibadilisha mwelekeo uliokuwa umechukuliwa na mtangulizi wake Rodrigo Duterte.

Baadhi ya taarifa katika ripoti hii inatokana na mashirika ya habari ya Reuters na AFP.

Forum

XS
SM
MD
LG