Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Januari 18, 2025 Local time: 17:33

China yaisihi UM kutumia sheria zake kuwajibisha mataifa juu ya hali ya hewa


China Jumanne imeieleza mahakama kubwa ya Umoja wa Mataifa kwamba mikataba ya sasa ya Umoja wa Mataifa inatoa misingi juu ya wajibu kisheria wa mataifa kukabiliana na kuongezeka kiwango cha joto, na athari za kuchangia kwao kwa muda mrefu tatizo hilo.

Baraza kuu la Umoja wa Mataifa, baada ya kampeni iliyoanzishwa na mataifa madogo ya visiwani kuitaka mahamaka ya kimataifa ya haki (ICJ), kutoa maoni yake juu ya nchi ambazo kisheria zinahusika na madhara mabaya ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Moja ya mataifa hayo Vanuatu, Jumatatu iliiomba mahakama kutambua madhila ya mabadiliko ya hali ya hewa, na kutaka kutolewa fidia kwa madhara hayo.

China moja ya mataiga mawili makubwa na Marekani yanayo changia hewa ukaa na kusababisha joto kuongezeka, imeeleza kutambua yale magumu mataifa yanayo endelea yanapitia.

Forum

XS
SM
MD
LG