Wizara ya Ulinzi ya taifa la Taiwan imesema ndege 82 za kijeshi za China zilivuka mstari wa kati wa mlango bahari wa Taiwan na nyingine zilikaribia sana njia ya maili 24 ambayo Taiwan huitumia kutambua eneo lake.
Mazoezi hayo ya kijeshi, yaliyopewa jina la “adhabu” kwa rais mpya wa Taiwan, Lai Ching-te, ambaye China inamwona kama mtu anayetaka kujitenga, yalilenga kufanya doria ya pamoja ya utayari wa kupambana katika anga, kukamata kwa pamoja udhibiti kamili wa uwanja wa vita, na mashambulizi ya usahihi ya pamoja kwenye malengo muhimu yanayohusisha majeshi ya China, ya wanamaji, anga na kikosi cha roketi.
Forum