Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Septemba 29, 2023 Local time: 20:07

China yafanya mazoezi ya kijeshi karibu na Taiwan


Picha iliyochukuliwa kutoka kanda ya video ya televisheni ya China, CCTV yaonyesha meli ya kivita ya China ikiendesha mazoezi ya kijeshi katika eneo karibu na Taiwan, Agosti 19, 2023.

China Jumamosi ilianzisha mazoezi ya kijeshi karibu na Taiwan kama “onyo kali kwa taifa hilo linalotaka kujitenga katika jibu la hasira lakini ambalo lilitarajiwa kwa kiasi kikubwa, kufuatia ziara ya makamu rais William Lai nchini Marekani.

Taipei imelaani mazoezi hayo ya China.

Lai, ambaye ni mgombea mkuu anayetarajiwa kuwa rais wa Taiwan katika uchaguzi wa Januari, alirudi nyumbani jana Ijumaa akitokea Marekani. Alifanya ziara rasmi fupi hapa Marekani akielekea na kutoka nchini Paraguay lakini hakutoa hotuba yoyote alipokuwa Marekani.

China inaichukulia Taiwan inayojitawala kidemokrasia kama himaya yake, licha ya upinzani mkali wa serikali ya kisiwa hicho.

Kamandi ya jeshi la China eneo la mashariki ilisema katika taarifa fupi kwamba, iliendesha mazoezi ya pamoja ya jeshi la majini na lile la anga karibu na kisiwa hicho.

Wizara ya ulinzi ya Taiwan imesema iligundua ndege 42 za China na meli nane zilizohusika katika mazoezi hayo karibu na kisiwa hicho kuanzia Jumamosi asubuhi na kwamba ilituma meli zake na ndege kukabiliana na hali hiyo.

Forum

XS
SM
MD
LG