Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Agosti 16, 2022 Local time: 01:04

China yaahidi Magufuli ushirikiano wa dhati kwa ajili ya maendeleo


JOHN MAGUFULI

Rais wa China Xi Jinping amesema kwamba China ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika mfumo mpana wa ushirikiano baina ya nchi hizo katika juhudi za maendeleo.

Xi amesema kwamba ushirikiano wa jadi kati ya China na Tanzania uliundwa na kujengwa na kizazi cha zamani, na kwamba China inajivunia ushirikiano wake na Tanzania kwa malengo ya maendeleo ya mda mrefu.

Amesema kwamba China itabaki kuwa rafiki mkubwa wa Tanzania hata iwapo mazingira ya uhusiano wa kimataifa na kiukanda utabadilika na kwamba China inaunga mkono sera ya Tanzania ya kutekeleza miradi yake ya maendeleo kwa kuzingatia hali yake ya kitaifa.

Xi amesisitiza kwamba China ipo tayari kushirikiana na Tanzania kwa njia mbalimbali ikiwemo kisiasa akiongezea kwamba China inasaidia taasisi zinazoekeza nchini Tanzania katika sekta za ujenzi, kilimo, viwanda miongoni mwa zingine.

Licha ya uhusiano wa miaka zaidi ya 50 baina ya Tanzania na China, awamu ya kwanza ya Rais Magufuli haikuonekana ikitilia mkazo historia ya ushirikiano wa nchi hizo.

Katika mazungumzo yao Xi alimpongeza pia rais John Magufuli kufuatia ushindi wake katika uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba.

Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG