Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 20:17

China: "Uhusiano wetu na Tanzania ni wakupigiwa mfano"


Wanawake wa Tanzania wakimkaribisha rais wa China, Xi Jinping, Machi 2013.
Wanawake wa Tanzania wakimkaribisha rais wa China, Xi Jinping, Machi 2013.

ripoti zinasema kuwa ushirikiano huo utaiwezesha Tanzania kuwa na viwanda vinavyokadiriwa kufikia 2000 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020.

Serikali ya Jamhuri ya watu wa China imesema mahusiano yaliyopo kati yake na Tanzania ni ya kupigiwa mfano.

Akiwa mwishoni mwa ziara yake ya siku moja nchini Tanzania Jumatatu, waziri wa mambo ya nje wa China, Wang Yi, amesema kuwa Tanzania ni mshirika wake wa karibu hivyo njia pekee ya kudhihirisha hilo ni kuendelea kwa pande hizo mbili kushirikiana katika nyanja za ukuzaji uchumi na maendeleo. Waziri huyo yuko ziarani barani Afrika.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili ya VOA, George Njogopa ameripoti kuwa China imesisitiza azimio lake la kudumisha uhusiano huo na imeahidi kuongeza kiwango chake cha uwekezaji nchini humo, ikianzia katika maeneo muhimu ikiwemo miundo mbinu, utamaduni na diplomasia.

Waziri huyo ameongeza kuwa nchi hizo zimekubaliana kuendelea kushirikiana katika maeneo yanayohusu miundo mbinu, uwekezaji wa biashara, elimu na maeneo mengine ya kidiplomasia.

Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje na sshirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt Augustine Mahiga amesema kuwa ushirikiano huo utafungua milango ya kukuza viwanda hasa wakati huu ambapo serikali ya awamu ya tano inahubiri kauli mbiu ya ujengaji viwanda.

Kwa mujibu wa afisa katika kitengo cha habari katika wizara hiyo, Mindi Kasiga viwanda hivyo vitajengwa kwa ushirikiano wa China na Tanzania.

Mwandishi wa VOA anasema hii ni mara ya pili katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kwa pande hizo mbili kusaini makubaliano ya ushirikiano wa kibiashara.

Makubaliano ya awali yaliyoshuhudiwa na rais wa China, Xi Jinping alipofanya ziara ya siku moja nchini Tanzania mwaka 2013 na kukutana na mwenyeji wake, rais wa wakati huo Jakaya Kikwete.

Hata hivyo Tanzania inaitazama China kama taifa linalokua kwa kasi katika uchumi wa dunia hivyo inaamini kuwa kupitia ushirikiano wao itaweza kusogeza mbele uchumi wake.

Ripoti zinasema kuwa ushirikiano huo utaiwezesha Tanzania kuwa na viwanda vinavyokadiriwa kufikia 2000 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2020.

XS
SM
MD
LG