Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 02:37

China kufanya vipimo vya covid kwa wakazi wa Shanghai, Ijumaa


Wakazi wa kitongoji cha Jing'an, Shanghai wakisibiri kupata vipimo vya covid Oktoba 25 , 2022.
Wakazi wa kitongoji cha Jing'an, Shanghai wakisibiri kupata vipimo vya covid Oktoba 25 , 2022.

Mji mkuu wa China wa Shanghai Ijumaa unafanya upimaji wa Covid-19 kwa wakazi wake  takriban milioni 1.3 kwenye kitongoji cha Yangou, huku watu wakitakiwa kubaki majumbani hadi matokeo yao yatakapojulikana.

Hatua hiyo inafuatia ile iliyochukuliwa wakati wa msimu wa joto, ya kufunga shughuli za kawaida kwa miezi miwili kwa wakazi wote milioni 25 mjini humo, suala lililoathiri pakubwa uchumi wake, kusababisha uhaba wa chakula pamoja na mizozo ya mara kwa mara kati ya wakazi na mamlaka. China haijaonyesha dalili za kulegeza masharti makali ya kukabiliana na janga hilo na hasa baada ya chama tawala cha kikomunisti kuongeza muda wa kiongozi wa taifa hilo Xi Jingping kwa muhula wa tatu wa miaka mitano. Kanuni kali za kudhibiti maambukizi ya covid zimewekwa kote China kuanzia Shanghai iliyoko upande wa mashariki hadi Tibet upande wa magharibi, ambako maandamano ya kupinga baadhi ya kanuni hizo yamekuwa yakishuhudiwa.

XS
SM
MD
LG