Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 23, 2023 Local time: 00:57

China kuanza kutoa visa baada ya kuondoa masharti ya Covid-19


China itaanza tena kutoa visa za aina zote na kufungua tena mipaka yake kwa watalii wa kigeni Jumatano, na kumaliza marufuku ya miaka mitatu iliyowekwa kupambana na janga la COVID-19.

Serikali Jumanne imesema kwamba utaratibu wa kuingia bila visa utaanza tena kwa maeneo kama vile kisiwa cha Hainan, na pia meli zinazoingia katika jiji la bandari kuu la Shanghai, ambazo hazikuwa na mahitaji ya visa kabla ya janga hilo.

Wageni ambao walipewa visa kabla ya Machi 28, 2020, wakati Beijing ilifunga mipaka yake kwa wageni, sasa wataruhusiwa kuzitumia kuingia nchini ilimradi hazijaisha muda wake.

Kuingia bila Visa pia kutaanza tena kwa wageni kutoka Hong Kong na Macau ikiwa pamoja kuingia jimbo la kusini la Guangdong.

Beijing, Desemba ilimaliza ghafla mkakati madhubuti wa kutokomeza kabisa Covid-19, uliowekwa kwa mara ya kwanza mwanzoni mwa janga hilo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG