Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 07, 2024 Local time: 11:23

China imeitaka Marekani kuchukua hatua kurekebisha makosa


Meng Wanzhou, mtendaji mkuu wa Huawei Technologies
Meng Wanzhou, mtendaji mkuu wa Huawei Technologies

Matamshi hayo yanafuatia kukamatwa kwa Meng Wanzhou ofisa mtendaji mkuu wa masuala ya fedha katika kampuni ya Huawei Technologies ya China

China imemuita balozi wa Marekani mjini Beijing siku ya Jumapili kuwasilisha ‘upinzani mkali’ juu ya kukamatwa kwa ofisa wa juu wa teknolojia wa China nchini Canada na Washington kutaka apelekwe Marekani ili kujibu mashtaka ya tuhuma za ubadhirifu.

Nembo ya Huawei Technologies
Nembo ya Huawei Technologies

China ilisema kukamatwa kwa Meng Wanzhou, ofisa mtendaji mkuu wa masuala ya fedha katika kampuni ya Huawei Technologies ni “jambo baya sana” na kuitaka Marekani ifute ombi lake la kutaka apelekwe nchini Marekani kwa kuhusishwa na shutuma kwamba alivunja sheria za Marekani ambazo zinapiga marufuku biashara na Iran.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa China, Le Yuchen amemuita balozi wa Marekani, Terry Branstad siku moja baada ya kumuita balozi wa Canada, John McCallum kupinga kukamatwa kwa Meng kwa ombi la Marekani kwenye uwanja wa ndege wa Vancouver hapo Disemba Mosi.

Wizara ya mambo ya nje ya China ilisema katika taarifa kwamba Le alimueleza Branstad “hatua za Marekani zinakiuka sheria na haki halali za raia wa China na kwa jinsi ilivyo ni mbaya sana.”

Beijing imeisihi Marekani “kuchukua hatua kurekebisha makosa, na kufuta hati ya kutaka kukamatwa dhidi ya raia wa China”.

Meng Wanzhou
Meng Wanzhou

Meng kama akipatikana na hatia nchini Marekani huenda akakabiliwa mpaka kifungo cha miaka 30 jela huku mwendesha mashtaka wa Canada alidai katika usikilizaji wa kesi hiyo siku ya Ijumaa mjini Vancouver kwamba Meng alitenda kosa mwaka 2013 kwa kuziambia taasisi za fedha kwamba kampuni ya Huawei ya China haina uhusiano na kampuni ya Skycom yenye makao yake Hong Kon ambayo ilikuwa ikiuza bidhaa za Marekani kwa Iran ikiwa ni ukiukaji wa vikwazo vya Marekani dhidi ya Tehran.

XS
SM
MD
LG