Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 09:15

Obama: Video ya Chicago inaonyesha 'uovu mkubwa' wa ubaguzi


Rais wa Marekani, Barack Obama alipotembelea Hyde Party Academy huko Chicago. Februari 2013.
Rais wa Marekani, Barack Obama alipotembelea Hyde Party Academy huko Chicago. Februari 2013.

hatunufaiki kukanusha kwamba hakuna ubaguzi na chuki, Hatunufaiki kuwa kuacha kuzungumza," amesema rais.

Rais wa Marekani, Barack Obama amesema video inayoonyesha vijana wanne wanaoshukiwa huko Chicago kumtesa kijana wa kizungu mwenye ulemavu wa akili “inatuwezesha kuona… “uovu mkubwa” wa ubaguzi, unyanyasaji na chuki vinavyoweza kuathiri familia na jamii.”

Washukiwa hao wameshtakiwa kwa uhalifu wa vitendo vya chuki baada ya kudaiwa kuwa walirekodi kitendo hicho cha uhalifu katika video na kuiweka kwenye Facebook kwa muda wa takriban nusu saa, wakionyesha jinsi wanavyompa mateso kijana huyo.

“Hatunufaiki kwa kukanusha kwamba hakuna ubaguzi na chuki. Hatunufaiki kwa kuacha kuzungumza,” amesema rais. “Ukweli ikiwa vitendo hivi vinajitokeza ina maana tunaweza kuvisitisha.”

Waendesha mashtaka katika kaunti ya Cook, huko Illinois, wametangaza Alhamisi mchana kuwa tuhuma za uhalifu wa chuki na utekaji nyara kwa nguvu ni makosa ambayo yanawakabili Jordan Hill, Brittany Covington na Tesfaye Cooper, wote wanaumri wa miaka 18, na Tanishia Covington, ana miaka 24.

Video hiyo inawaonyesha vijana hao wamarekani weusi wakiendeleza shambulizi na kumpiga ngumi kijana wa kizungu ambaye hakuweza kutambulika baada ya kumfunga na kumziba kinywa chake.

Video hiyo pia inaonyesha washambuliaji hao wakimlazimisha kijana mwenye tatizo la akili kunywa maji kutoka chooni na kuzikata baadhi ya nywele zake kichwani kabla ya kumwagia majivu kwenye jeraha lililokuwa linavuja damu.

Wakati wote ilipokuwa inarekodiwa video hiyo, washambuliaji hao wanasikika wakimtukana kijana huyo kwa kelele na kukashifu watu weupe na rais mteule Donald Trump. Katika hatua moja, washambuliaji hao walimlazimisha kijana mnyonge huyo kusema maneno machafu dhidi ya Trump.

Kwa mujibu wa polisi, mtu huyo alishikiliwa kati ya saa 24 na 48 kabla ya polisi wa doria kumuona, pale walipokuwa wakizunguka katika eneo hilo ambapo tukio hilo lilitokea.

Mara polisi walipomuona, kijana huyo alichukuliwa hospitali na kutambuliwa kama mtu ambaye taarifa za kupotea kwake zilisha sambaa katika mji jirani.

Mmoja kati ya watesaji wake, alikuwa ni mwanafunzi mwenzie na alimdanganya afuatane naye, polisi wamesema.

XS
SM
MD
LG