Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 11:04

Cheptegei wa Uganda ashinda dhahabu katika mbio za nyika za IAAF


Mwanariadha raia wa Uganda, Kiprui Cheptegei
Mwanariadha raia wa Uganda, Kiprui Cheptegei

Mwanariadha raia wa Uganda, Jumamosi alishinda dhahabu katika mbio za nyika za watu wazima kwenye mashindano ya kimataifa ya riadha, IAAF yaliyofanyika mjini Aarus, nchini Denmark.

Joshua Kiprui Cheptegei, lishinda kwa kumaliza mbio hizo kwa dakika 31 na sekunde 40 akifuatiwa na mwenzake kutoka nchi hiyo hiyo, Jacob Kiplimo, aliyechukua dakika 31 na sekunde 44 kumaliza mbio hizo.

Geoffrey Kipsang Kamworor wa Kenya, ambaye ndiye alikuwa anashikilia taji hilo, alichukua nafasi ya tatu.

Cheptegei amekuwa raia wa Kwanza wa Uganda kuibuka mshindi kwenye mbio hizo za IAAF.

Katika mashindano ya IAAF yaliyofanyika nchini Uganda mwaka wa 2017, mwanaridha huyo hakuwa kwa orodha ya kumi bora katika mbio hizo, na ushindi wake wa Jumaosi umetajwa kama wa kushangaza.

Kwa upande wa wanawake, Mkenya Hellen Obiri, aliibuka mshindi kwa kuchukua dakika 36 na sekunde 14. Dera Didam alikuwa wa pili na dakika 36 sekunde 16, huku nafasi ya tatu ikichukuliwa na Letesenbet Gidey wa Ethiopia.

XS
SM
MD
LG