Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Februari 16, 2025 Local time: 17:48

Chebukati akataa kuwarejesha makamishna wa IEBC kazini


Mwenyekiti Wafula Chebukati
Mwenyekiti Wafula Chebukati

Makamishna wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Kenya waliokuwa wamejiuzulu April hawataweza kurudi kazini kwa sababu walifanya hivyo kwa uamuzi wa kudumu kwa kufuata sheria na taratibu za kikazi, Mwenyekiti wa Tume Wafula Chebukati amesema.

Katika tamko lake alilotuma kwa vyombo vya habari, Chebukati amekataa kuwarejesha kazini aliyekuwa makamu wa mwenyekiti Consolata Maina na Kamishna Margaret Mwachanya akisema kuwa walifuata utaratibu wa kuacha kazi IEBC na katiba.

IEBC Commissioners who resigned in April cannot resume office because they did so irrevocably by following legal and official procedures, the commission's chair Wafula Chebukati says. ALSO READ: Mudavadi wants resuming IEBC commissioners charged In his statement sent to newsrooms, Mr Chebukati has rejected the resumption of office by former vice chair Consolata Maina and Commissioner Margaret Mwachanya pointing to their adherence to IEBC resignation procedures and the constitution.
Read more at: https://www.standardmedia.co.ke/article/2001293548/chebukati-why-commissioners-cannot-resume-their-positions

Mwenyekiti Chebukati amekataa kata kata kuwaruhusu kurejelea majukumu yao na kusisitiza kuwa tume hiyo haina afisi za kuwarudisha wafanyakazi wa zamani.

Margaret Mwachanya na Consolata Nkatha Maina ambao walibisha hodi kwenye afisi za IEBC, walijiuzulu Aprili 16 kwa madai kuwa mwenyekiti wa tume hiyo alikuwa ameshindwa kuiongoza tume hiyo ipasavyo. Lakini kurejea kwao kazini sasa kumeibuwa hisia chungu nzima.

Makamishna hao walisisitiza kuwa hawakuwa na imani na Chebukati na uongozi wake.

Aidha, walisisitiza kuwa Chebukati hakuwa na uwezo wa kuiimarisha tume wakati panapokuwapo na maoni tofauti. Na vile vile kurudisha rasilimali za IEBC; Magari,simu, tarakilishi, kadi za bima, na kadhalika.

Hata hivyo kiini cha kurejea kwao kazini ni uamuzi wa Jaji Wilfrida Okwany wa Mahakama Kuu wa Agosti 14, ulioleza kuwa makamishna hawa watatu hawakujiuzulu ipasavyo kisheria.

Watatu hawa walikuwa wamewasilisha mahakamani hati za viapo kueleza kuwa walijiuzulu ipasavyo kwa kumuandikia Rais Uhuru Kenyatta barua za kujiuzulu.

Kauli ambayo mpaka sasa haijathibitishwa kwani Rais Kenyatta hajaelezea iwapo aliidhinisha kujiuzulu kwao au la.

Chebukati anasisitiza kuwa nafasi zao hazipo tena. Na iwapo wanataka kumuona itabidi wamwandikie barua rasmi ya kuomba nafasi ya mazungumzo.

Mwanasheria George Kithi anaeleza kuwa haipo sheria inayomkinga kamishna yeyote wa IEBC kurejelea majukumu yake.

Wakili Kithi anasisitiza kuwa wawili hawa walitelekeza majukumu yao na hivyo basi hawafai kurejea kazi hiyo wakati wamekuwa nje ya afisi zao kwa kipindi cha miezi tano.

Kiongozi wa Amani National Congress Musalia Mudavadi anasema kuwa haifai kuwaruhusu maafisa hawa wa awali wa IEBC kurejea kazini.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Kennedy Wandera, Kenya

XS
SM
MD
LG