Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor amepanga kukata rufaa juu ya hukumu iliyotolewa kwenye kesi yake kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu.
Mahakama maalum kwa ajili ya Sierra Leone ilitoa taarifa fupi jumanne ikisema mawakili wa utetezi wa Taylor wameandika waraka wa nia ya kukata rufaa.
Mahakama ilimhukumu Taylor mwenye umri wa miaka 50 kwenda jela mwezi uliopita kwa kuwasaidia waasi Sierra Leonne ambao wamefanya ukatili wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo.
Majaji walimkuta na hatia kwa makosa yote 11 ambayo yalihusisha mauaji, ubakaji, utumwa wa ngono na kuandikisha askari watoto.
Mahakama ilisema Taylor alikuwa hana amri juu ya waasi lakini alikuwa anajua shughuli zao na kuwapa silaha na vitu vingine.