Afghanistan ni moja na mataifa mawili ulimwenguni ikiwemo jirani yake Pakistan ambako ugonjwa huo usiotibika unaendelea kupooza watoto.
Maafisa wa afya kutoka mataifa yote mawili wametangaza kesi moja kila mmoja mwaka huu ikiwa idadi ndogo zaidi kuwahi kutangazwa ikilinganishwa na visa 84 vya Pakistan 56 vya Afghanistan mwaka uliopita. Kampeni ya utoaji chanjo ya nyumba kwa nyumba itaanza Novemba 8 ikilenga kufikia takriban watoto milioni 10 walioko chini ya umri wa miaka 5 kote nchini humo.
Miongoni mwa watoto wanaolengwa ni wale takriban milioni 3 wanaoishi kwenye maeneo ambayo hayangefikiwa awali, kulingana na shirika la afya duniani WHO. Taliban ambao walichukua madaraka ya Afghanistan mwezi Agosti awali walikuwa wamepiga marufuku utoaji wa chanjo kwenye maeneo walikoshikiliwa mwaka wa 2018, wakati wa makabiliano dhidi ya serikali ya rais Ashraf Ghani iliyoanguka.
Facebook Forum