Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 03:59

Chanjo ya Polio yazua mdahalo Nigeria


Mama na watoto wake wakiwa katika hospitali moja huko Nigeria.
Mama na watoto wake wakiwa katika hospitali moja huko Nigeria.

Suala la chanjo ya polio linajadiliwa katika mdahalo wa katiba ya Nigeria kama serikali inaweza kulazimisha chanjo bila ruhusa ya wazazi.

Mdahalo wa katiba unaendelea huko Nigeria kubaini ikiwa serikali inaweza kushitaki wazazi ambao wanakataa watoto wao kupewa chanjo dhidi ya polio, au ikiwa ina nguvu ya kulazimisha wazazi kuwapeleka wanao kupewa chanjo dhidi ya magonjwa yoyote ile ya kuambukiza.

Mdahalo huo umetokea baada ya serikali ya jimbo la Kano huko Nigeria kusema itamshitaki mzazi yeyote anayemkataza mtoto wake kupewa chanjo hiyo kwa mdomo kuzuia mojawapo ya magonjwa hatari ya kuambukiza.Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kifungu cha katiba ya Nigeria kinalinda haki ya wanigeria wote kuwa na faragha ikiwa ni pamoja na faragha ya masuala ya afya yao na haki ya kukataa matibabu.

Lakini mawakili wanaowakilisha shirika la huduma za afya nchini humo wanaeleza kwamba kifungu kingine kinaipa serikali haki ya kuingilia wakati afya na maisha ya raia yako hatarini na kuwapa watoto wote chanjo bila kuomba ruhusa ya wazai wao.

XS
SM
MD
LG