Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 29, 2024 Local time: 18:21

Chanjo ya malaria yatoa matumaini kwa watoto


Mtoto akipata chanjo ya majaribio ya malaria katika mji wa Kilifi nchini Kenya.
Mtoto akipata chanjo ya majaribio ya malaria katika mji wa Kilifi nchini Kenya.

Malaria inasababisha ugonjwa kwa watu millioni 200 kila mwaka na kuuwa karibu watu laki nane, wengi wao watoto barani Afrika.

Chanjo mpya ya majaribio ya ugonjwa wa malaria, kwa mara ya kwanza, imeonyesha kuwa salama kuweza kutumika kuepusha ugonjwa huo kwa watoto wadogo, watafiti waliripoti Jumanne.

Matokeo ya utafiti huo ambayo yalikuwa yakisubiriwa kwa hamu yalihusisha zaidi ya watoto wachanga elfu 15 na wengine chini ya miaka mitano katika nchi saba za Afrika. Matokeo hayo yanaonyesha kuwa chanjo hiyo inaweza kupunguza kwa nusu nzima uwezekano wa kupata malaria, na kwa theluthi moja nzima uwezekano wa kufa kutokana na ugonjwa huo.

Watafiti hapo awali waliripoti matokeo kutokana na idadi ndogo ya washiriki katika utafiti huo katika nchi za Tanzania, Kenya, Msumbiji, Gabon na Ghana.

Lakini ripoti hii mpya inaonyesha matokeo kutoka watoto wote 15,460 walioshirikishwa katika utafiti huo katika nchi zilizotajwa hapo juu pamoja na Malawi na Burkina Faso katika utafiti uliofanywa kati ya Marchi 2009 na Januari 2011.

Chanjo hiyo inayojulikana kama RTS,S inatengenezwa kwa ushirikiano wa taasisi moja isiyo ya kiserikali ya PATH iliyoko Seattle nchini Marekani na kampuni ya kutengeneza madawa ya GlaxoSmithKline pia ya Marekani. Taasisi ya Gates Foundation pia ya Seattle Marekani ilichangia dolla millioni 200 katika gharama ya utafiti huo.

XS
SM
MD
LG