Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Aprili 23, 2024 Local time: 22:59

Kampuni ya Sanofi kushiriki kutengeneza chanjo ya Zika


Kampuni ya kutengeneza madawa ya Sanofi kutoka Ufaransa imesema leo kuwa itashirikiana na jeshi la Marekani katika kutengeneza chanjo dhidi kirusi cha Zika.

Taasisi ya kijeshi ya Walter Reed itatoa habari kwa kampuni hiyo ya Ufaransa kutokana utafiti mpya uliofanywa ukionesha chanjo dhidi ya virusi vya Zika ikifanya kazi kwenye mwili wa panya.

Mwaka uliopita, kampuni ya Sanofi ilitengeneza chanjo dhidi ya homa ya ndengue inayoenezwa na mbu wanaoeneza Zika.

Ugonjwa wa Zika umekuwa ukishuhudiwa hasa Brazil ambapo takriban watu milioni 1.5 wameambukizwa tangu ulipotokea mwaka jana.

Wanawake wajawazito walioambukizwa Zika mara nyingi wanajifungua watoto walio na vichwa vidogo kuliko kawaida. Hali hiyo inajulikana kama microcephaly na kumekuwa na kesi 1,600 zilizoripotiwa Brazil kufikia sasa.

XS
SM
MD
LG