Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 21, 2024 Local time: 08:04

Changamoto za kuishi kwenye makazi duni Nairobi


Muuza miwa akikpita katika kitongoji cha Kibera, makazi duni ya karibu watu 1 million katika mji mkuu wa Kenya wa Nairobi.
Muuza miwa akikpita katika kitongoji cha Kibera, makazi duni ya karibu watu 1 million katika mji mkuu wa Kenya wa Nairobi.

Takriban asilimia sitini ya watu wanaoishi jijini Nairobi, Kenya wanaishi katika makazi duni kwenye vijibanda.

Maisha katika mitaa hii ambapo watu wanaishi kwenye vijibanda ni yenye kukatisha tamaa na vile vile yanahofisha mno.

Wakazi wengi wanaelezea changamoto kubwa ni kupata lishe bora, nafasi bora za elimu, maji safi pamoja na usalama wa kutosha.

Hilo bado ni tatizo kwao hata baada ya serikali ya nchi hiyo kuanzisha mfumo wa kuboresha mitaa hiyo.

Kuna Faraja

Lakini kuna faraja kubwa baada ya kuwa katika eneo hili, zipo taasisi mbalimbali za kibinafsi zinazotoa elimu, makazi na hata huduma za kiafya kwa jamii ambazo baadhi ya wakazi wake hujikuta wakijihusisha na madawa ya kulevya.

Watoto kati ya umri wa miaka sita hadi saba wakiwa darasani Kibera, Nairobi.
Watoto kati ya umri wa miaka sita hadi saba wakiwa darasani Kibera, Nairobi.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA Kennedy Wandera hivi karibuni alipotembelea kituo cha watoto yatima cha Cheryl’s children’s home alijionea jinsi ambavyowatoto mbalimbali wanaendelea kupata huduma muhimu kujiendeleza kimaisha.

Anasimulia kuwa kupitia mpango wa serikali wa kujenga na kuimarisha mitaa duni nchini ambayo ni makao ya watu takriban milioni tano nukta tatu, watu wengi katika maeneo hayo wanatarajia kupata makazi bora, huduma bora za kiafya itapofika mwaka 2030.

Mchakato Umeanza

Lakini mpango huu bado uko kwenye mchakato, baadhi ya mitaa ya duni hapa jijini Nairobi, imeendelea kushuhudia kipindi kigumu ambapo matumizi ya dawa za kulevya, ndoa za mapema zimeathari jamii hizo.

Katika mtaa wa Dagorretti Corner hatua chache kutoka barabara ya Ngong, pamejengwa kituo cha watoto kijulikanacho kama Cheryl’s Children’s Home and Learning Centre. Katika kituo hiki binafsi, watoto yatima kutoka mitaa duni mbalimbali wenye kuishi vibandani wametengenezewa mabweni na madarasa kama hatua muhimu ya maendeleo ya jamii kupitia elimu bora.

Kituo hiki cha watoto yatima ambacho kilianzishwa mwaka 1997 na mumewe ambaye alifariki kwa ugonjwa wa saratani, hivi sasa kina zaidi ya watoto mia moja hamsini.

Kwa sasa kituo hiki kinafadhili wanafunzi kumi na wawili katika vyuo vikuu. Wengi wa watoto hawa wamepitia hali ngumu za maisha baada ya kuwapoteza wazazi wao kupitia ugonjwa wa ukimwi

Mama anaihi na HIV katika kitongoji cha Kibera
Mama anaihi na HIV katika kitongoji cha Kibera

Rai ya Umma

Hata hivyo, Mary Sigei ambaye ni mfanyakazi katika kituo hiki ameeleza kuwa watoto wengi kutoka jamii za mitaa ya mabanda huathirika pakubwa na matatizo mengi ya kifamilia lakini Cheryl’s huwapa matumaini wanapojisajili hapa.

Gilbert Magagani, ni mzazi ambaye licha ya changamoto za maisha, alifanikiwa kumsajili mtoto wake katika kituo hiki. Bwana Magagani ameeleza kuwa jamii katika mitaa hii ya mabanda hupitia katika hali ngumu na hivyo basi ni vyema kuwepo kwa vituo muhimu.

Edith Odhiambo ni mzazi katika kituo hiki cha Cheryl’s Children’s Home and Learning Centre. Edith anaeleza kuwa watoto wengi wametelekezwa na jamii zao na vile vile kukiri kuwa yapo matatizo makubwa ambayo watoto hao hupitia.

XS
SM
MD
LG