Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 02:16

Dunia yakabiliana na changamoto za ujinga na dijitali


Mradi wa kidijitali elimu ya ngumbaro nchini Kenya
Mradi wa kidijitali elimu ya ngumbaro nchini Kenya

Siku ya Ijumaa (septemba 8) imeadhimishwa Kimataifa kupinga ujinga wa kutojua kusoma na kuandika ambapo kauli mbinu ya mwaka huu ni “kusoma na kuandika katika dunia ya kidijitali”.

Wakati wa shamra shamra hizo wanakisomo wameonekana nchini Kenya na sehemu nyingine duniani wakifuarahia namna mfumo wa dijitali umerahisha mbinu za kutuma ujumbe na kutuma pesa.

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO linasema katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hii teknolojia za kidijitali zinaendelea kupenya katika nyanja zote za maisha na kuathiri namna watu wanavyoishi, kujifunza na kushirikiana na jamii.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti kuwa zaidi ya vituo elfu sita vya masomo ya watu wazima na wanakisomo zaidi ya laki mbili wanapokea masomo ya kujua kusoma na kuandika huku wengine wakipata fursa ya kujiendelza ili kufikia malemngo endelevu ya maendeleo kitengo cha nne kuhusu elimu kwa wote.

Kuambatana na kauli mbiu ya mwaka huu ya siku hii ya kimataifa yalikuwepo maonyesho ya moja ya vituo vya elimu ya watu wazima ya Bombolulu Mombasa inayotoa mafunzo ya teknolojia.

Grace Wambete ni mwalimu wa darasa ataja kuwa matumizi ya simu na utandawazi yamepunguza migogoro ya kifamilia ikilinganishwa na enzi za matumzi ya barua hasa kwa wale walishindwa kujisomea na kusaidiwa na majirani.

Hata hivyo elimu hiyo ya watu wazima nchini bado inakumbwa na changamoto za madarasa na walimu katika kufikia wote wanaohitaji masomo yao huku tamaduni zikichangia mabibi kunyimwa fursa ya kuendelea na masomo hayo nchini kama anavyoeleza mama Mnyazi.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu Amina Chombo, Kenya.

XS
SM
MD
LG