Wakati huo, rais wa sasa Muhammadu Buhari atakuwa akikamilisha ,muda wake baada ya kuhudumu kwa mihula miwili yenye jumla ya miaka 8, kwenye taifa hilo lenye idadi kubwa zaidi ya watu barani Afrika, na lenye wingi wa mfuta ghafi.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, Buhari kinyume na viongozi wengi wa Afrika hajamtaja mridhi wake, na kwa hivyo kuwacha nafasi hiyo ikiwa wazi.
Tinubu mwenye umri wa miaka 70 ameshinda wagombea wengine 13 kwenye kura za mchujo wa chama cha All Progressives Congress,APC. Kiongozi huyo alipata wajumbe 1,271 akilinganishwa na mshindani wake wa karibu aliyepata wajumbe 316 pekee.
Facebook Forum