Chama cha Leba kimeshinda viti hivyo, ikiwa ni changamoto kwa utawala wa waziri mkuu Rishi Sunak na chama chake wakati Uingereza inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Matokeo hayo ya uchaguzi mdogo ni ya hivi punde kwa chama kinachotawala kupoteza viti kwa chama cha upinzani, na chama cha Leba sasa kina matumaini kwamba huenda kikapata ushindi katika uchaguzi mkuu ujao baada ya kuwa chama kikuu cha upinzani kwa muda wa miaka 14.
Chama cha Leba kilikuwa na matumaini madogo ya kushinda viti hivyo vya Tamworth na Bedfordshire, katikati mwa Uingereza, ambazo ni ngome za chama cha Conservative.
Viti hivyo vilibaki wazi baada ya wabunge wake kujiuzulu, mmoja wao kutokana na madai ya kashfa ya ngono.
Uingereza inakabiliwa na hali ngumu ya uchumi, gharama ya juu ya maisha na chama cha Conservative kimekuwa kikikabiliwa na sakata za kila mara.
Forum