Chama cha SPLM kinachoongozwa na makamu rais Riek Machar, kimejiondoa kwenye utaratibu wa ufuatiliaji wa amani, ili kupinga kuendelea kwa mashambulizi kwenye vituo vyake, yanayoendeshwa na mshirika wake wa kusaka amani, chama hicho kimesema.
“Hatuoni maana ya kuendelea kushiriki katika mikutano isiyoleta manufaa yoyote ambapo masuala yanawasilishwa lakini hayatatuliwi”, chama hicho kimesema katika taarifa.
“Maeneo yetu yanashambuliwa na mshirika wetu wa kusaka amani bila hatua yoyote kuchukuliwa na wale waliopewa majukumu ya kuwajibisha wahusika wa ukiukwaji huo”, chama hicho kimesema, kikiongeza kuwa, shambulio la hivi karibuni lilifanyika Jumatatu kaskazini mashariki mwa nchi.
Kujiondoa huko kwa SPLM kunaongeza mgwanyiko kati ya makundi yanayomtii Machar na rais Salva Kiir ambayo yalipelekea utekelezaji wa makubaliano ya amani ya mwaka wa 2018 yaliyomaliza mapigano kati ya wanaume hao wawili.
Sudan Kusini, ilikabiliwa na ukosefu wa usalama tangu ijipatie uhuru mwaka wa 2011, na kumaliza karibu nusu ya uwepo wake kama taifa lenye vita.