Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 06, 2022 Local time: 23:35

Chama kikuu cha upinzani India chapata kiongozi mpya


Kiongozi wa muda wa chama cha Congress Party Sonia Gandhi (kushoto) akimpa shada la maua kiongozi mpya wa chama hicho aliyechaguliwa Mallikarjun Kharge mjini New Delhi, India, Oktoba19, 2022.

Chama kikuu cha upinzani cha India cha Congress kimemchagua kiongozi mpya kutoka nje ya familia ya Nehru-Gandhi.

Hii ni mara ya kwanza baada ya kipindi cha zaidi ya miongo miwili wakati kikijaribu kuboresha hali yake ya kisiasa ambayo imegauka sana toka chama cha kizalendo cha Kihindu cha Janata kuchukuwa madaraka mwaka 2014.

Mallikarjun Kharge veterani wa siku nyingi wa chama hicho na waziri wa zamani wa serekali kuu atachukuwa madaraka kutoka kwa kiongozi wa sasa wa muda Sonia Gandhi.

Kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 80 alipata asilimia 80 ya kura zilizopigwa na wajumbe wa chama cha Congress 9,300, na kumshinda mpinzani wake kirahisi Shashi Tharoor mwanachama wa bunge na mwanadiplomasia wa zamani wa Umoja wa Mataifa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG