Kiongozi wa chama kidogo cha kisiasa cha Taiwan ambaye amekuwa katika mazungumzo na chama kikuu cha upinzani kwa tiketi ya pamoja ya urais hakuonyesha dalili zozote za kusalimu amri siku ya Jumapili katika mzozo uliozuka kuhusu nani agombee urais na nani awanie makamu wa rais.
Suala la China, ambayo inaiona Taiwan kama eneo lake, linagubika uchaguzi wa Januari 13 wa wabunge na urais. China imeongeza shinikizo la kijeshi na kisiasa, ikiwa ni pamoja na mazoezi ya kivita ya hali ya juu, kushinikiza kisiwa hicho kukubali madai ya kujitawala ambayo Taiwan inakataa.
Baada ya majuma kadhaa ya mazungumzo makali sana juu ya kujiunga kwenye uchaguzi wa rais, Kuomintang (KMT) na chama kidogo zaidi cha Taiwan People's Party (TPP) walikubaliana Jumatano kuangalia jumla ya kura za maoni ili kuamua mgombea wa chama gani atasimama kugombea kama rais na nani kama makamu wake.
Forum