Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 10, 2023 Local time: 04:10

Chama cha upinzani Uganda kupinga pendekezo la sheria.


Rais Yoweri Museveni wa Uganda.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

Chama kikubwa cha upinzani nchini Uganda kimesema kitapinga pendekezo la sheria inayowapa polisi madaraka ya kusimamia mikutano ya hadhara.

Chama cha upinzani Uganda kupinga pendekezo la sheria.

Chama kikubwa cha upinzani nchini Uganda kimesema kitapinga pendekezo la sheria inayowapa polisi madaraka ya kusimamia mikutano ya hadhara.

Msemaji wa chama cha forum for democratic change, Wafula Oguttu, amesema kuwa sheria hiyo iko nje ya katiba na ina lengo la kukandamiza upinzani kabla ya uchaguzi mwaka 2011.

Amesema chama hicho kitapinga sheria hiyo mahakamani kama itapitishwa na bunge. Chini ya pendekezo la mswada huo makundi yatatakiwa kuiarifu polisi kabla ya kufanya mkutano wowote wa hadhara au maandamano.

Makundi ya kutetea haki za binadamu huko Uganda pia yamepinga pendekezo a sheria hiyo yakisema kuwa itakiuka haki za kiraia. sheria hiyo inapitiwa na baraza la mawazili na baadae itapelekwa katika bunge kwa ajili ya kupitishwa.

Uganda inatarajiwa kufanya uchaguzi wa ubunge na urais februari mwakani. Rais Yoweri museveni ameongoza Uganda tangu aliponyakua madaraka mwaka 1986. Tangu hapo ameshinda chaguzi tatu wa hivi karibuni ikiwa mwaka 2006 .

XS
SM
MD
LG