Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 24, 2024 Local time: 02:10

Tume huru ni muhimu kushinda uchaguzi Zanzibar


Kiongozi wa chama cha upinzani cha CUF, Seif Shariff Hamad.
Kiongozi wa chama cha upinzani cha CUF, Seif Shariff Hamad.

Kiongozi wa chama cha upinzani cha CUF kisiwani Zanzibar amesema vyama vyenye nguvu vya upinzani vinahitajika pamoja na tume ya uchaguzi ilio huru ili kushinda marais walioko madarakani.

Seif Shariff Hamad ameongeza kuwa waafrika lazima wahakikishe kuwa jeshi pamoja na vikosi vingine vya usalama vinawekwa mbali na siasa kwa kuwa mara nyingi vinatumika kusaidia chama tawala.

Maalim Seif Sharif azungumza na Abdushakur
please wait

No media source currently available

0:00 0:10:42 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Zanzibar ni kisiwa ambacho ni sehemu ya Tanzania pamoja na visiwa vingine viwili, vidogo kwenye Bahari Hindi karibu na ufukwe wa Tanzania.

Mwezi Machi mwaka huu, Zanzibar ilifanya uchaguzi wa marudio ya uchaguzi wa Oktoba mwaka jana lakini chama cha CUF kilisusia kwa kuwa kiliamini kuwa mgombea wake Hamad alikuwa ameshinda kwenye uchaguzi wa awali.

Hamad sasa hivi yuko kwenye ziara hapa mjini Washington kukutana na viongozi wa Marekani kuhusu hali ya kisiasa ya Zanzibar.

XS
SM
MD
LG