Akihutubia mkutano wa chama tawala cha Scotland katika mji wa Dundee, Yousaf aliapa kuwa ataanzisha mazungumzo mapya na serikali ya ufalme wa Uingereza kuhusu uhuru ikiwa chama chake cha SNP kitashinda viti vingi zaidi vya nchini humo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwakani.
“Niseme wazi, SNP ikishinda uchaguzi huu, wananchi watakuwa wamezungumza,” alisema.
"Tutatafuta mazungumzo na serikali ya ufalme wa Uingereza kuhusu jinsi tunavyo changia katika demokrasia kwa Scotland kuwa taifa huru.”
Matamshi ya Yousaf yanakuja huku uungwaji mkono wa umma ukipungua kwa chama cha SNP baada ya kukamatwa kwa kiongozi wake wa zamani na waziri wa kwanza Nicola Sturgeon, kiongozi mkuu wa harakati za kudai uhuru katika miaka ya hivi karibuni.
Mkutano wa Dundee ni mkutano wa kwanza wa ana kwa ana tangu Yousaf, 38, achukue nafasi yake mwezi Machi, na chama kilianza kuona mteremko mkubwa katika umaarufu wake.
Forum