Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 16:17

Chama cha Repablikan kimeshinda na kutwaa udhibiti wa bunge


Chama cha Republikan kimeshinda na kuchukuwa udhibiti wa baraza la wawakilishi Jumanato.

Hatua hiyo inatoa nguvu kwa Warepablikan ndani ya Washington, pamoja na kuwapatia wahafidhina fursa ya kukabili ajenda za rais wa Marekani, Joe Biden, na kuendesha mfululizo wa uchunguzi.

Ikiwa ni zaidi ya wiki moja toka uchaguzi kufanyika, Warepablikan wamefikisha viti 218 vinavyo hitajika kuchukuwa udhibiti wa baraza ambalo linashikiliwa na Wademokrat.

Hali halisi ya wingi wao katika baraza hautaonekana kikamilifu mpaka siku ama wiki kadhaa kuputa, wakati ambapo sasa kura katika maeneo yenye ushindani zinaendelea kuhesabiwa.

Ushindi huu umekuja ikiwa ni saa kadhaa baada ya rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump kutangaza nia ya kugombania urais katika uchaguzi wa mwaka 2024 kupitia chama cha Republikan licha ya kuwepo upinzani mkali dhidi yake.

XS
SM
MD
LG