Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 21:42

Chama cha MDC chashinda kiti cha Spika wa bunge.


Chama cha MDC kikisheherekea ushindi wa Lovemore Moyo kuwa tena spika wa bunge.
Chama cha MDC kikisheherekea ushindi wa Lovemore Moyo kuwa tena spika wa bunge.

Mbunge wa ngazi ya juu wa chama cha MDC ambaye pia ni waziri wa nishati bado yupo gerezani.

Hali ya wasiwasi ilitanda katika mji mkuu wa Zimbabwe Harare Jumanne, huku chama cha Waziri Mkuu Morgan Tsvangirai Movement For Democratic Party kikishinda kile cha Bw. Mugabe ZANU-PF katika uchaguzi wa spika wa bunge.

Mwandishi wa VOA Peta Thornycroft anaripoti kuwa uchaguzi huo ulikuwa wa ushindani mkubwa huku baadhi ya wabunge wakiwa wamefungwa jela wakati wa kura hiyo.

Spika wa zamani Lovemore Moyo anayefahamika kwa uungaji mkono wake kwa chama cha Bw. Tsvangirai alishinda tena kiti hicho, kura hiyo ikiashiria kuwa baadhi ya wabunge kutoka chama cha Bw. Mugabe walimpigia kura.

Chama hicho cha MDC kilishinda kile cha ZANU-PF katika uchaguzi wa wabunge mwaka wa 2008.

Uchaguzi wa Jumanne wa spika la bunge ulifuatia maamuzi ya mahakama kuu ya Zimbabwe kuwa kuchaguliwa kwa Bw. Moyo katika uchaguzi wa kwanza mwaka wa 2009 hakukuwa halali, na hivyo ikabidi uchaguzi wa kiti hicho ufanyike tena.

Na ingawa dazeni za wabunge kutoka vyama vyote vitatu wameaga dunia tangu mwaka wa 2008, makubaliano ya kisiasa katika serikali ya Umoja wa Kitaifa yanapiga marufuku uchaguzi mdogo.

ZANU-PF ilimteuwa mwenyekiti wa chama Simon Khaya kugombania kiti cha Spika, huku Bw. Tsvangirai akiamua kumteuwa tena Lovemore Moyo ambaye pia ni mwenyekiti wa chama chake.

Chama kidogo kilichojitenga na chama cha MDC kinachoongozwa na Welshman Ncube hakikumteuwa mgombea na kilikuwa kimeahidi kuwa wabunge wake hawatashiriki katika kura hiyo. Lakini Jumatatu chama hicho cha Ncube kiliamua kumuunga mnkono Lovemore Moyo kikisema kuwa kukamatwa kwa wabunge wa chama cha Bw. Tsvangirai umehujumu demokrasia.

Mbunge wa ngazi ya juu wa chama cha MDC ambaye bado yuko gerezani ni waziri wa nishati Elton Mangoma aliyekamatwa Ijumaa iliyopita. Mangoma ana ulemavu wa miguu na huchechemea anapotembea.

Hata hivyo kulikuwa na shamra shamra baada ya chama cha upinzani MDC kushinda kiti hicho cha spika wa bunge la Zimbabwe.

XS
SM
MD
LG