Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 04, 2023 Local time: 07:19

Chama cha Macron bado chaongoza Ufaransa


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mkewe Brigitte Macron wakipiga kura Jumapili
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na mkewe Brigitte Macron wakipiga kura Jumapili

Chama cha rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron, kisichokuwa na uzoefu kinaelekea kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi wa bunge nchini humo.

Tayari matokeo ya duru ya kwanza ya upigaji kura Jumapili yanaonyesha kuwa chama hicho kimeshinda kwa asilimia 28 ya kura.

Matokeo hayo ya chama cha La Republique en Marche, na chama mshirika wake cha MoDem, ambacho kilikuwa na asilimia 4 ya kura, kinafanya vyama hivyo kupata zaidi ya viti 400 katika baraza kuu la bunge lenyeviti 577, iwapo mafanikio yao yataendeleahadi kwenye raundi ya mwisho ya uchaguzi huo itakayofanyika wiki ijayo.

Hata hivyo, idadi ya wapiga kura ilikuwa chini mno jana Jumapili, huku asilimia 52 ya wapiga kura wakisusia uchaguzi.

“Mimi nilikuwa namfagilia zaidi mgombea wa Republik katika harakati za uchaguzi (Chama cha Rais Emmanuel Macron) lakini kuna uhalali katika hili inapokuwa zaidi ya asilimia 50 ya wapiga kura walisusia kupiga kura, achilia mbali wale waliokuwa wameamua kuacha karatasi za kura bila ya kujaza kitu. Hakika, hili linatuleta karibu na ushindi, lakini nafikiri kuna suala kubwa zaidi juu ya uhalali wake kisheria.

Chama cha Republik kilichokuwa kikiwania ushindi, ambacho kiliundwa mwaka mmoja ili kumwezesha Macron kushinda, kiliwaweka katika nafasi ya wagombeaji idadi ya wagombea ambao walikuwa hawajulikani kitu ambacho sio cha kawaida.

Chama cha Conservative Les Republicains kinatarajiwa kuunda ni ngome kubwa ya pili katika Bunge la Taifa na kutabiriwa kuwa itapata viti kati ya 95-125.

XS
SM
MD
LG