Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Februari 09, 2023 Local time: 02:39

CHADEMA yaeleza sababu za kumpeleka Tundu Lissu Kenya


Mbunge wa Singida mashariki, Tundu Lissu

Mbunge wa Singida mashariki na Rais wa chama cha mawakili Tanganyika Tundu Lissu aliyeshambuliwa kwa kupigwa risasi na kujeruhiwa Alhamis katika mkoa wa Dodoma huko Tanzania hivi sasa anapatiwa matibabu zaidi ya afya yake katika nchi jirani ya Kenya.

Chama cha upinzani Tanzania cha CHADEMA kupitia katibu Mkuu wake Dr.Vincent Mashinji kilieleza sababu mojawapo iliyopelekea Tundu Lissu kupelekwa mjini Nairobi nchini kenya kwa matibabu ni kutokana na hali ya mazingira ya usalama wake ikijumuisha namna tukio lenyewe lilivyotokea na mahala ambapo tukio hilo limefanyika na hivyo kama chama waliona ni vyema kiongozi na mwanachama mwenzao asafirishwe nchi jirani kwa msaada zaidi wa matibabu.

Sauti ya Amerika-VOA ilizungumza na Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA kwa Zanzibar, Salumu Mwalimu kuhusu tukio hilo la kushambuliwa kwa risasi na kujeruhiwa kwa Tundu Lissu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:37 0:00

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG