Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 20:41

Chadema wamkabidhi barua rasmi Zitto


Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini
Zitto Kabwe, mbunge wa Kigoma Kaskazini
Nchini Tanzania mgogoro ndani ya chama kikuu cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA umeingia katika hatua nyingine baada ya chama sasa kukabidhi rasmi barua za tuhuma kwa wanachama wake watatu waandamizi waliovuliwa nyadhifa za uongozi hivi karibuni, akiwemo mbunge wa kigoma kaskazini Zitto Kabwe.

please wait

No media source currently available

0:00 0:02:37 0:00
Kiungo cha moja kwa moja

Akizumgumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, mwanasheria mkuu wa CHADEMA, bwana Tundu Lissu amesema aliyekuwa naibu katibu mkuu wa chama hicho, bwana Zito Kabwe, pamoja na mjumbe wa kamati kuu ya CHADEMA, Dk.Kitila Mkumbo na mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba wataitwa mbele ya Kamati Kuu ya chama hicho kujitetea kabla ya maamuzi ya mwisho dhidi yao kufikiwa hivyo hakuna sababu ya kujadili kwa sasa hatma ya wanachama hao.

Hata hivyo bwana Lissu amesisitiza kwamba wanachama hao waandamizi waliokuwa wakishikilia nyadhifa muhimu za uongozi ndani ya CHADEMA wamevuliwa nyadhifa hizo kutokana na kupanga mpango wa mapinduzi ya uongozi wa juu jambo ambalo amesema ni kinyume na katiba, maadili na itifaki ya CHADEMA na hivyo kukanusha alichokiita upotoshaji uliofanywa na watuhumiwa hao kwenye maelezo yao.

Kwa upande wake mkurugenzi wa habari wa CHADEMA, John Myika amesisitiza kuwa hatma ya kisiasa ya wanachama hao machachari ndani ya chama hicho iko mikononi mwa kamati kuu ndani ya siku 14 baada ya utetezi wao.

Aidha kuhusiana kwamba Zitto Kabwe ana adhibiwa kwa kuonyesha nia ya kuwania uongozi wa juu wa chama hicho, Tundu Lissu ameseama CHADEMA mwaka jana kiliweka mwongozo wa wananchama wake wanaotaka kuwania nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya chama ili kuepuka migongano na hivyo wanaokwenda kinyume wanakiuka taratibu.
XS
SM
MD
LG