Majeshi ya Chad, yamevurumusha wanamgambo wa Boko Haram, kutoka mji wa Dikwa, kaskazini mashariki mwa Nigeria, na kupoteza mwanajeshi mmoja katika mapambano kwa mujibu wa msemaji wa jeshi.
Shirika la habari la Reteuters linaripoti kwamba Chad imepeleka maelfu ya wanajeshi wake katika maeneo muhimu kuzunguka ziwa Chad.
Hizo ni hatua za kupambana na wanamgambo wenye msimamo mkali ndani ya Nigeria, na wakati mwengine kuvuka mipaka.
Hatua hiyo imechochewa toka wanamgambo wa Boko Haram, waliposhambulia kijiji cha Chad, cha Ngouboua, mwezi uliopita na kuua watu kadhaa katika shambulio la kwanza kufahamika lililosababisha vifo nchini humo