Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Julai 18, 2024 Local time: 18:05

Chad yakomboa mji wa Dikwa kutoka kwa Boko Haram


Wanajeshi wa Chad wakiwa katika doria
Wanajeshi wa Chad wakiwa katika doria

Vikosi vya Chad, katika mji wa Dikwa, kaskazini mashariki mwa Nigeria, vinasema vimekomboa tena mji huo kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram.

Jeshi limeripoti kwamba wanajeshi 34 walijeruhiwa katika juhudi za kuukomboa mji huo ambao ulikuwa chini ya Boko Haram kwa wiki kadhaa.

Wanajeshi walikwenda mtaa kwa mtaa kutafuta wanamgambo waliosalia ama kushindwa kukimbia.

Shirika la habari la Associated Press linasema mamia ya raia wa Dikwa, katika jimbo la Borno, waliuwawa wakati wanamgambo hao walipoushikilia mji huo.

Idhaa ya Sauti ya Amerika ya Hausa inaripoti kwamba wakimbizi kutoka katika mji huo wamekuwa wakihofia kuzungumzia kile kilichotokea.

Shirika la wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) Jumanne limesema wakimbizi 16,000 waliomba hifadhi nchini Cameroon baada ya kutoroka mapigano ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.

XS
SM
MD
LG