Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 04, 2022 Local time: 11:00

CHAD: Waasi wajiondoa katika mazungumzo ya amani


Rais wa serikali ya mpito nchini Chad Mahamat Idriss Deby PICHA: AFP

Kundi kubwa la waasi limejiondoa katika mazungumzo ya amani ya Chad, yanayoendelea Qatar.

Mazungumzo ya amani yamekuwa yakiendelea kati ya makundi ya wapiganaji na uongozi wa kijeshi, tangu kifo cha rais Idriss Deby aliyeuawa akiwa katika mapigano mieizi 10 iliyopita.

Kundi la waasi linalojiita Baraza la kijeshi kwa ajili ya ukombozi wa jamhuri ya Chad CCMSR, ambalo linatekeleza sana shughuli zake kusini mwa Libya na kaskazini mwa Chad, limetanga kujiondoa kwa mazungumzo hayo, likisema kwamba serikali ya kijeshi ina lengo lisiloeleweka vyema

Generali Mahamat Idriss Deby, mwenye umri wa miaka 38, na ambaye alichukua hatamu za uongozi wa Chad baada ya kifo cha babake, amesema kwamba lengo lake kuu ni kuleta makundi yote ya waasi pamoja kwa ajili ya mazungumzo na kumaliza mgogoro nchini humo.

Mazungumzo yamepangiwa kuanza rasmi May 10.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG