Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Februari 23, 2024 Local time: 05:41

Catalonia wanataka kujitenga kutoka Spain


Wapiga kura wa Catalonia wakitumia haki yao
Wapiga kura wa Catalonia wakitumia haki yao

Msemaji wa serikali kwenye eneo Jordi Turull alisema kura milioni 2.02 kati ya kura zilizopigwa milioni 2.26 walipendelea uhuru. Rais wa Catalan, Carles Puigdemont alisema awali atatangaza peke yake uhuru kutoka Spain kama matokeo yanaonesha zaidi ya asilimia 50 ya wapiga kura wanataka kujitenga.

Wafuasi na bendera za Catalonia wakiunga mkono kujitenga
Wafuasi na bendera za Catalonia wakiunga mkono kujitenga

“Tumepata haki ya kuwa na taifa ambalo litakuwa jamhuri”, Puigdemont alisema katika hotuba kwa njia ya televisheni baada ya vituo vya kupigia kura kufungwa. Serikali ya Spain hata hivyo haikubaliani na hilo.

Maafisa huko Catalan walisema zaidi ya watu 800 walijeruhiwa wakati polisi walipojaribu kuwazuia wakazi kupiga kura. Mahakama ya katiba ya Spain ilisimamisha sheria iliyopitishwa na bunge kwenye eneo likitoa wito wa upigaji kura lakini kura ya maoni ilifanyika licha ya hali hiyo kuwepo.

XS
SM
MD
LG