Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 05, 2024 Local time: 07:27

Mcheza filamu ya Star Wars afariki


Mcheza filamu Carrie Fisher.
Mcheza filamu Carrie Fisher.

Carrie Fisher ambae alipata umaarufu wa kimataifa kwa kucheza nafasi ya Princess Leia kwenye filamu ya Star Wars amefariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 60.

Carrie Fisher ambae alipata umaarufu wa kimataifa kwa kucheza nafasi ya Princess Leia kwenye filamu ya Star Wars amefariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 60. Fisher alipata shinikizo la moyo wiki iliopita akiwa kwenye ndege kuelekea Los Angeles dakika 15 kabla ya kutua.

Mtaalam wa afya aliekuwa kwenye ndege hiyo alimpa huduma ya kwanza hadi pale alipopelekwa hospitalini baada ya ndege kutua ambapo kufikia Jumapili familia yake ilisema kuwa hali yake ilikuwa imeimarika. Hata hivyo Jumanne bintiye Billie Lourd alitoa taarifa kupitia msemaji wake kuhusu kifo cha Fisher.

Kando na filamu ya Star Wars, Fisher pia atakumbukwa kwa kucheza kwenye Austin Powers, The Blue Brothers, Hannah and Her Sisters na When Harry Met Sally.

XS
SM
MD
LG