Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 15, 2024 Local time: 04:36

Carrie Lam hatagombea mhula wa 2 Hong Kong


Kiongozi mkuu wa Hong Kong Carrie Lam akiondoka kwennye jukwaa baada ya kuzungumza na wandishi wa habari April 4 2022. Picha Reuters
Kiongozi mkuu wa Hong Kong Carrie Lam akiondoka kwennye jukwaa baada ya kuzungumza na wandishi wa habari April 4 2022. Picha Reuters

Kiongozi mkuu wa Hong Kong Carrie Lam ametangaza kwamba hatagombea muhula wa pili madarakani.

Akizungumza na waandishi wa habari, Lam amesema kwamba anataka kushughulikia maswala ya familia yake.

Lam amesema kwamba atakamilisha mhula wake wa miaka mitano June 30 mwaka huu na kuhitimisha huduma yake kwa serikali ya Hong Kong, ambayo ametumikia kwa mda wa miaka 40, katika nafasi mbalimbali.

Amesema kwamba alijulisha utawala wa China bara kwamba hatagombea mhula mwingine madarakani, mwanzoni mwa mwaka 2021, na kwamba wamemuelewa.

Vyombo vy ahabari vya Hong Kong vimekuwa vikiandika habari kwamba John Lee, ambaye ni afisa wa ngazi ya juu katika utawala wa mji huo wa kibiashara, huenda akajiuzulu nafasi yake ya sasa na kugombea nafasi ya juu ya usimamizi wake.

Uchaguzi wa Hong Kong, ambao ulikuwa umepangiwa kufanyika March 22, uliahirishwa hadi May 8 kutokana na maambukizi mapya ya virusi vya Corona.

Kiongozi wa Hong Kong huchaguliwa na kamati ya watu 1,500, wakiwemo mawakili na waakilishi wa biashara, pamoja na amakundi mengine ya wataalam.

XS
SM
MD
LG