Mti wa Krimasi kwenye bunge la Marekani mwaka huu wenye urefu wa mita 24 kutokaJimbo la Idaho uliwashwa taa Jumanne jioni kwenye bustani ya magharibi ya jumba hilo maarufu kama Capitol Hill hapa Washington.
Mti wa mwaka huu kufuatana na utamaduni ulioanza mwaka wa 1964 ulikatwa kutoka msitu wa kitaifa wa Payette karibu na mji wa McCall katika jimbo la Idaho. Mti huo wenye umri wa miaka 84 ulikatwa Novemba 2 na kufika hapa Washington siku 26 baadaye.
Bendi ya jeshi la anga la Marekani ilicheza nyimbo za Krismasi wakati wa sherehe hiyo huku spika wa bunge Paul Ryan na Isabella Gerard ambae ni mwanafuzi wa darasa la 5 kutoka Boise Idaho wakiwasha taa za kwenye mti huo. Isabella alikuwa miongoni mwa wanafunzi 200 walioshiriki kwenye mashindano ya kuhudhuria hafla hiyo.
Facebook Forum