Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 22, 2024 Local time: 17:17

Hatimaye, ni Ghana, Ivory Coast katika fainali


Licha ya fujo zilizotaka kuharibu mechi Ghana ilitoka na ushindi wa kishindo dhidi ya wenyeji Equatorial Guinea kuingia fainali

Ghana na Ivory Coast ndio zitakutana katika fainali ya kombe la mataifa Afrika 2015 Jumapili, Februari 8 mjini Bata. Ghana ilijikatia tiketi ya fainali kwa kuwachapa wenyeji Equatorial Guinea 3-0 katika mechi ya pili ya nusu fainali Alhamisi.

Ivory Coast ndio ilikuwa ya kwanza kuingia fainali baada ya kuichapa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo - DRC - 3-1 katika nusu fainali ya kwanza Jumatano.

Ghana ilipata bao la kwanza katika mechi yao dhidi ya Equatorial Guinea kwa njia ya penalti katika dakika ya 42 pale Jordan Ayew alipachika penalti ya kiulaini kabisa baada ya golikipa kumvamia mshambuliaji wa Ghana.

Dakika chache baada kabla ya halftime Wakaso aliipatia Ghana bao la pili baada ya kupokea krosi nzuri ambayo alidhibiti kwa guu la kulia na kumwacha mlinzi wa Equatorial Guinea kando na kupachika bao safi kimiani.

Katika nusu ya pili Equatorial Guinea walinza kuonekana kuchanganyikiwa kwa uchezaji wa hasira hapa na pale na hali hiyo ilifungua fursa nyingine kwa Ghana kupata bao la tatu katika dakika ya 75 ambalo lilifungwa na Andre Ayew.

Mechi ilisimamishwa kwa dakika kadha zikiwa zimebaki kiasi cha dakika saba kutokana na ghasia zilizoanzia katika stendi wa watizamaji ambao inaelekea walikuwa wakitupa chupa na mawe uwanjani. Baada ya muda mchezo ulirejea uwanjani lakini hadi wakati huo mshindi alikuwa wazi.

Wachambuzi wa kandanda Afrika wanasema fainali hii ni ile ambayo wamekuwa wakiotea kwa muda mrefu baina ya Ghana na Ivory Coast - timu ambazo zina wachezaji kadha katika ligi za Ulaya.

XS
SM
MD
LG