Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 20, 2023 Local time: 19:47

Cameroon: Washukiwa kadhaa wa mauaji ya mwanahabari mashuhuri wakamatwa


Rais wa Cameroon Paul Biya

Polisi nchini Cameroon wamewakamata watu kadhaa wanaoshukiwa kuhusika katika utekaji nyara, mateso na mauaji ya mwanahabari mashuhuri wa radio, ofisi ya rais wa Cameroon imesema Alhamisi.

Martinez Zogo, mwenye umri wa miaka 50, ambaye aliweka hadharani kashfa ya udanganyifu wa kifedha na urafiki wa kimapenzi serikalini katika taifa hilo la Afrika ya kati, alitekwa nyara tarehe 17 Januari nje ya kituo cha polisi katika vitongoji vya mji mkuu Yaounde.

Mwili wake ambao ulikuwa umekatakatwa vibaya ulipatikana siku tano baadaye.

Rais Paul Biya, ambaye ameitawala kimabavu Cameroon kwa zaidi ya miaka 40, aliomba uchunguzi wa pamoja wa jeshi la polisi na maafisa wengine wa usalama juu ya mauaji hayo.

“Uchunguzi umefanikisha kukamatwa kwa watu kadhaa ambao kuhusika kwao katika uhalifu huu wa kuchukiza kunashukiwa vikali,” waziri wa utawala na katibu mkuu kwenye ofisi ya rais Ferdinand Ngoh Ngoh amesema Alhamisi.

Taarifa yake imesema msako wa washukiwa wengine ulikuwa ukiendelea.

Takriban watu 20 mashuhuri wa Cameroon Alhamisi waliandika katika gazeti la Ufaransa Le Monde, kuhusu “wasiwasi wao mkubwa juu ya hali ya uhasama inayojitokeza kwenye mjadala wa umma” nchini humo.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG