Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Juni 20, 2024 Local time: 14:25

Jeshi la Cameroon laachilia watu 12 waliotekwa na waasi


Wanajeshi wa Cameroon wakipiga doria.
Wanajeshi wa Cameroon wakipiga doria.

Kanali Asoualai Blama, ambaye aliongoza operesheni ya kuachiliwa huru kwa mateka, amewataka raia kuripoti kuhusu wageni wasio wafahamu waliokuwa kwenye jamii zao.

Jeshi la Cameroon limewaachilia watu 12 wanaoshikiliwa mateka na washukiwa waasi takriban 30 kwenye mpaka wake na taifa lililokumbwa na ghasia la Jamhuriya Afrika ya Kati. Jeshi la Cameroon linasema kuwa wawili kati ya waasi hao waliuwawa na wanajeshi kadhaa walijeruhiwa katika operesheni saa 48.

Gavana wa mkoa wa Adamawa nchini Cameroon anasema kuwa watu 12 ikiwa ni pamoja na watoto, waliachiliwa huru baada ya jeshi ya Cameroon kufanya operesheni kwenye mpaka wake na jamhuri ya afrika ya kati.

Kildadis Taguieke Boucar anasema, kwa bahati mbaya, baadhi ya watekaji nyara waliweza kutorokea katika nchi jirani.

Anasema washambuliaji walitambuliwa upesi na raia na jeshi la Cameroon kwa sababu walikuwa wamevalia sare za jeshi la kigeni , ishara kwamba waasi wengi na watenda maovu walitokea nchi za nje, bado walikuwa wanafanya operesheni ndani ya Cameroon.

Miongoni mwa mateka waloachiliwa huru walisafirishwa na jeshi la Cameroon kutoka eneo la mpakani hadi uwanja wa ndege wa Ngaoundere katika mkoa wa Adamawa ni mfugaji ngombe mwenye umri wa miaka 47, Mohammadu Njobdji, ambaye anasema alikuwa matekani kwa mda wa wiki mbili baada ya kutekwa pamoja na watoto wake wawili kutoka nyumbani kwao huko Ngaoui.

Mohammadu anasema siku alipotekwa nyara kulikuwa na sauti kubwa ya kubisha mlango kama saa 5 usiku, huku sauti zikimtisha iwapo atakataa kufungua mlango, basi yeye na familia yake watauwawa. Anasema alipofungua mlango baadhi ya watu walokuwa wamejificha nyuso zao, na walokuwa wamevalia mavazi meusi wakiwa wamejihami kwa silaha, waliwaamrisha wote kuwafwata.

Njobji anasema, walipokuwa wametekwa katika eneo la milima la mpakani, waliambiwa kulipa fidia ya hadi dola elfu 10 kila mmoja wao ili wapate kuachiliwa. Anasema walipigwa kila asubuhi na kulishwa nyama kutoka kwa ng’ombe walioibiwa.

Kanali Asoualai Blama, ambaye aliongoza operesheni hiyo ya kuachiliwa huru kwa mateka, amewataka raia kuripoti kuhusu wageni wasio wafahamu waliokuwa kwenye jamii zao. Anasema jeshi la Cameroon lina azma ya kupambana na washambuliaji, lakini vita hivyo haviwezi kushindwa bila kushirikisha raia.

XS
SM
MD
LG