Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Novemba 28, 2022 Local time: 08:24

Cameroon imefanya uchaguzi wa urais


Mpigakura Cameroon akitumia haki yake ya kidemokrasia

Taifa la Cameroon lilishuhudia matukio kadhaa ya ghasia Jumapili wakati upigaji kura ulipoanza katika uchaguzi uliotarajiwa kwa kiasi kikubwa kuongeza muda wa utawala wa Rais Paul Biya, mmoja wa viongozi wa Afrika aliye madarakani kwa muda mrefu.

Shirika la habari la Reuters lilieleza kwamba zoezi la upigaji kura lilifanyika salama kwa sehemu kubwa ya taifa hilo la Afrika ya kati lililopo katika mgawanyiko wa lugha na kupelekea baadhi ya vituo vya kupiga kura kutofunguliwa katika maeneo ya Anglophone na kuzusha ghasia.

Watu takribani watatu waliokuwa na silaha kwenye eneo linalojitenga walifyatuliwa risasi na kuuwawa na vikosi vya usalama huko kaskazini mashariki katika mji wa Bamenda unaozungumza lugha ya ki-Ingereza, chanzo kimoja cha usalama kilisema.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG