Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Oktoba 08, 2022 Local time: 00:43

Mamia waokolowa kutoka kwa Boko Haram


Watu walotekwa na Boko Haram , walookolewa na jeshi la Cameroon wawasili Maroua, Cameroon.

Katika kipindi cha miezi miwili iliopita, vikosi vya Nigeria na Cameroon vimewaokoa mamia ya watu kutoka Nigeria waliokuwa wameshikwa mateka na wanamgambo wa Boko Haram. Wengi wao sasa wanaishi kwenye kambi zilizo wazi katika mji wa Kolofata ulioko kaskazini mwa Cameroon.

Upepo mkali unavuma kwenye kambi ya muda ya Sabongari ambacho ni kijiji kilichoko kwenye mpka nje ya mji wa Kolofata. Kambi hiyo sasa ni makazi ya zaidi ya watu 800 waliotoroshwa makwao na mzozo wa Boko Haram.

Miongoni mwao ni mwanamke wa umri wa miaka 56 Dada Aminatou. Alitoroka kutoka kijiji chake kilichoko karibu na mji wa Banki chini ya umabali wa kilomita 20 kutoka hapa wakati wa uvamizi uliotekelezwa na jeshi la Cameroon mwezi huu.

Aminata anasema Boko Haram hawangewaruhusu kutoka nyumbani. Mali zao na ng’ombe zilichukuliwa. Anasema wanamgambo waliwachukua wavulana wote na kuwapeleka kwenye kambi zao ndani ya msitu. Anasema kuwa yeye pamoja na wanakijiji wengine walitoroka wakati uvamizi wa bunduki ukiendelea kutoka jeshi la Cameroon. Anasema baadhi ya wapiganaji wa Boko Haram waliweza kutoroka huku wengine wakiuwawa au kukamatwa. Anasema wanakijiji waliomba wanajeshi hao kuwapeleka Cameroon kutokana na hofu kuwa wanamgambo wangerudi kulipiza kisasi.

Aninatou anasema baadhi ya wanakijiji hawajulikani walipo ikiaminika huenda waliuwawa wakati wa mapigano. Anasema jeshi la Cameroon halikusaidia walioumia.

Baadhi ya wanaigeria waliokoseshwa makao wanalaumu vikosi vya Cameroon kwa kuwachomea nyumba na kuuwa zaidi ya watu 150 wakati wa operesheni hiyo, jambo ambalo serikali ya Cameroon imekanusha.

Akama Ngeti ambae ni kamanda wa wa jeshi la Cmeroon mjini kolofata anasema uperesheni imefanikiwa na itaendelea hadi pale Boko Haram watakapoangamizwa.

Habari njema ni kuwa, hatukupoteza mwanajeshi hata mmoja hapa. Tumeuwa wanachama wa Boko Haram wengi. Kwa sasa, tumeshikilia eneo lote bila matatizo. Hali sasa ni tulivu.

Afisaa huyo amesema wote waliokuwa mateka watbaki kwenye kmabi za uhamisho hadi pale vijiji vyao vitakapokuwa salama, lakini mazungumzo yanaendelea na serikali ya Nigeria kuwarudisha makwao. Serikali ya Cameroon na mashirika ya kutoa misaada wanashughulikia mahitaji ya watu hao waliokuwa wametekwa wengi wao wakisema wananuia kubaki kwenye kambi hizo kwa wakati huu.

XS
SM
MD
LG